07/11/2022
JINSI MITUME WA YESU WALIVYOKUFA
Mathayo - Alikufa kwa kuuwawa kwa upanga mbali kidogo na mji wa Ethopia.
Marko - Alikufa kule Alexandria baada ya kukokotwa kikatili kwenye barabara ya mji.
Luka - Alitundikwa juu ya mti wa mizeituni katika nchi ya Kigiriki ya kimaendeleo.
Yohana - Alitiwa kwenye p**a la mafuta yanayochemka lakini hakufa kwa njia ya miujiza na baadaye akapelekwa kwenye Kisiwa cha Patimo ili afe hata hivyo hakufa huko. Alikufa huko Efeso miaka 100 BK.
Petro – Alisulubiwa kule Rumi kichwa chini miguu juu mwaka 67 BK.
Yakobo Zebedayo – Alikatwa kichwa kule Yerusalemu mwaka 44 BK, Mdo 12:1-2.
Yakobo wa Alifayo – Alitupwa kutoka kwenywe kinara na kisha kupigwa na rungu
lenye misumari mpaka kufa, mwaka 62 BK.
Batholomayo – Alichunwa ngozi akiwa hai mpaka akafa.
Andrea – Alifungwa kwenye msalaba huku akiendelea kuwahubiria wale watesi
wake mpaka kufa.
Thomaso – Alishindiliwa mkuki ndani ya mwili kule Klemandel nchi
ya India ya mashariki.
Yuda Thadayo – Alipigwa kwa mkuki mpaka akafa.
Barnaba wa Mataifa – Alipigwa kwa mawe kule Thesolonike.
Mathayo – Kwanza alipigwa kwa muda mrefu na baadaye akakatwa kichwa.
Paulo – Aliteswa kwa muda mrefu na baadaye kukatwa kichwa kule
Rumi na Mfalme Nero mwaka 67 BK.
Kitu kikubwa kilichowasukuma hawa wapendwa hata hawakuogopa kifo, ni Imani waliyokuwa nayo. Hawakukiogopa kifo kwa sababu walijua kwamba Yesu waliekuwa nae alikishinda kifo na kaburi. Yesu alipowapa utume hawakurudi nyuma kamwe, walitawanyika katika mataifa na miji mbali mbali, wakilihubiri Neno la Mungu. Leo Mungu anahitaji watu majarisi k**a hao, watu wasiokata tamaa, watakao kuwa tayari kwenda popote na kufanya lolote mbingu itakalowatuma. Ingawa watakumbana na upinzani, kutokueleweka, kutukanwa na kudharauliwa, lakini daima watainua vichwa vyao juu na kumtazama yeye alie watuma.