15/01/2018
with ・・・
Nikiwa na miaka 14 mtu angeniambia nitakuja kuweza kuongea sentensi mbili kamilifu ningebisha. Nilikuwa na kigugumizi kilichohatarisha sio tu mazungumzo na watu lakini zaidi confidence yangu. Bado nina kigugumizi mpaka leo. Lakini nikaanza kuzingatia jinsi ya kujicontrol, jinsi ya kujilazimisha maneno yatoke. Kwa yeyote mwenye hili tatizo anajua huu mchakato ulivyo mgumu pale maneno yakienda kujibanza somewhere kati ya koo na kinywa 😂. Matokeo yake: Naongea sana na mikono, kuna wakati naongea haraka maana inabidi nilidake neno fasta kabla flow haijapotea 🙆🏽, nyakati nyingine nakaa kimya na saa nyingine naitikia au nakataa kwa kichwa. Point is niko conscious. Ukianza kuwa mkweli na udhaifu wako utaanza kuzingatia maeneo ya kuweza kujiboresha na kutafuta mbinu za kutumia. Leo hii nasimama mbele za watu na kutoa sauti yenye maneno. Kwa uliyewahi kunisikia nikiongea na ukanielewa ujue tu matunda ya jitihada zangu ni wewe, ni kwasababu nilitaka usikie kilicho ndani yangu. Napambana na mimi mwenyewe, kesho niwe bora kuliko leo. Kila kitu ukiweka nia, inawezekana. Weka nia, kuwa na bidii, utaweza.
👌